Monday, 26 May 2014
JIONEE MAMBO YA BI. SAIDA KATIKA NDOA YAKE
Ndoa ya Bi. Saida iliyofungiwa nyumbani kwao Tabata na kumalizikia nyumbani kwa Mume Mbezi ilipendeza sana kama wao wenyewe walipendeza sana Allah awajaalie maisha marefu na kizazi chema...
ALLY POWER: KUNA BAADHI YA WASANII WA MAZAUG NIKIFANYA NAO KAZI HUWA NI BURUDAAAAAAAANIII
DIRECTOR Na Camera Man Mkuu wa Faiz Media, Ally Power, Amesikika akiwasifia hadharani baadhi ya waimbaji wa kaswida wa kikundi cha MAZAUG kuwa ni rahisi kufanya nao kazi hususan wakati wa kushoot, kwa madai kuwa ni wepesi wa kufuata maelekezo kwa muda mfupi.
Akieleza hayo baada ya kumalizika kwa shughuli ya upigaji picha katika moja ya locations jijini DAR, Director Huyo makini, aliamua kuyatoa ya moyoni na kueleza ni jinsi gani anafurahishwa na umakini unaoonyeshwa na baadhi ya wasanii wa kundi hilo wakati wa zoezi zima la kurekodi.
''Unajua bwana, hakuna kitu kizuri kama kufanya kazi na mtu ambae yupo smart. Mtu mwenye kipaji halisi na mwelewa. Ni raha sana kwa kuwa unaokoa muda na unapata kitu tarajiwa'' alisema Ally Power
Alipoulizwa kwanini anasema hivyo na ni wasanii gani ambao anapata nao urahisi wakiwa locations, bila kumung'unya maneno aliwataja na kuwamwagia sifa kemkem,
''Kuna hawa mabinti wawili kwakweli me huwa naenjoy sana ninapokuwa nao ONSET, Nao ni
Husna Masanza na Asha Kivoja naskia hata kwenye audio recording pia wako fresh sana, big up kwao, hata kazi zao zinathibitisha haya''
Katika Hatua nyingine, Muongozaji huyo ambae pia ni Editor mzuri wa Videos, amewalalamikia baadhi ya wana-kikundi kwa kile anachodai kuwa hawapo makini na hawazingatii yale anayowaelekeza, hivyo kupelekea kutia ugumu kazi ambayo hulazimika kufanya kwa muda mrefu na kupoteza muda pasipo na sababu za msingi.
Akizidi kufunguka, Ally Power anasema kuna wakati huwa anapata tabu na kuchoka kuwapa maelekezo baadhi ya waimbaji kwa kuwa hawako 'serious' na kile wanachokifanya, kitu ambacho anadai huwa kinamkera na kulazimika kufanya kazi kwa msongo 'stress'!
''Inachosha sana kufanya kazi na mtu / watu ambao naweza kusema hawajielewi! Utakuta script ipo wazi, inamwelekeza mtu nafasi yake ya ku-cover, unampa na maelekezo mafupi tu ili kupata picha na tukio zuri, eti mtu anaanza kujichekesha kusiko na msingi na kuleta poz mara sijui jua kali...ooh siwez kusimama muda mrefu...aargh...inaboa '''' Alinukuliwa akilalamika Muongozaji huyo.
Katika hali ya kushangaza alipoulizwa kwa upande wa wanaume, alijibu kwa ufupi mno, ''Hao hawana matatizo, Wote Ni MAJEMBE''
MOJA YA KAZI ZA FAIZMEDIA PRODUCTION!!!
SONG: KISHORLELA
ARTIST : H KELLY FEAT SHABBYTONE
DIRECTOR: ALLY POWER / FAIZMEDIA PRO
STUDIO: KUKAYA RECORDS / DA' HERO ( SNAKE)
Friday, 23 May 2014
Tuesday, 20 May 2014
NDANI YA KITCHEN PARTY YA BI. SAIDA MAMBO YALIKUWA HIVI.....
Ndani ya kitchen party ya Bi. Saida iliyofanyikia katika ukumbi wa Highland jijini dar es salaam sherehe iliyofana sana na yenye kupendeza wakiongozwa na Bi. harusi wetu mtarajiwa Faiz Media tulikuwa nao bega kwa bega kuhakikisha mambo yanakwenda sawiya pa Barakati Kimangele akiwa katika swala zima la Decoration
JIONEE MAMBO YALIVYOKUWA.....
Saturday, 10 May 2014
MAGOGONI MUSLIM GRADUATION
Naam ni siku nyingine tena tukiwa pamoja na Mc Massanza katika kazi ya mahafali ya kuhitim kwa wanachuo wa TPSC (Magogoni) kwa ngazi ya cheti na diploma.
KWA MATUKIO ZAIDI BOFYA HAPA
Friday, 2 May 2014
NDOA YA BI. FADHILA URASA
Ndoa ya Bi. fadhila Urasa iliyofanyikia nyumbani kwao kimara chini ya Faiz Media sherehe ambayo ilipendeza sana na watu wengi walifurahi saaana na ilifana sana.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Subscribe to:
Posts (Atom)