Naitwa Fadhili Massanza nina umri wa miaka 29 mzaliwa wa Kilimanjaro Mwanga - Ugweno. mwenyeji wa Dar es saalam - Ilala - Buguruni Mnyamani.
Napenda sana kufanya shughuli zangu ndogondogo na nnapenda sana kuimba (QASWIDA).
Kusikiliza mambo mbalimbali ya kiuchumi na kidini.
Napenda sana kuishi na watu wa rika tofauti tofauti na wenye upeo mbalimbali kwani huwa ni mwongozo katika maisha yangu hasa pale ninapojifunza na kuyachukuwa mazuri kutoka kwao.
Napenda vijana wenzangu hasa wenye hari ya kujituma na kuhangaika kwa ajili ya kesho yao na familia zao.

Napenda kutoa nasaha zangu kwa vijana wote wake kwa waume tujitahidi kupambana vita dhidi ya umaskini na ufukara kwani hata Mungu ametuusia kupambana navyo vyote.
Hakuna njia yeyote kujikwamua zaidi ya kufanya kazi kwa juhudi na pia kuelekeza nguvu na maombi kwa Mungu pekee katika yote tunayo yafanya kwani

"Mungu humpa amtakaye bila ya hesabu"
Nawapenda nyote RAMADHAN QAREEM
No comments:
Post a Comment