Thursday, 24 July 2014

SHEREHE YA HARUSI YA BW. FADHIRI NA BI.AKANASHE AT MASAI CLUB

Sherehe ya Bw. Fadhiri Ng'unda na Bi. Akanashe Swai iliyofanyika Masai Club ilikuwa ni sherehe ya aninayake watu walikula, kunywa, walicheza na kufarahi pamoja na wawili hao walikuwa wakitimiza jambo kubwa na adwim kabisa la ndoa.
Usipitwe na matukio japo kwa uchache upate kujionea mambo yalivyokuwa ndani ya ukumbi kwa kubofaya HAPA

Monday, 14 July 2014

USIKOSE UZINDUZI WA DUNIA - KILIMANJARO !



HODI! HODI! KILIMANJARO ! ! ! EID MOSIIII......!!

''''''MAZAUG WANAKUJA KUANDIKA HISTORIA''''''

KAMPUNI YA FAIZ MEDIA ( www.facebook.com/faizmedia )
IKISHIRIKIANA NA POWER VISION TANZANIA
( www.facebook.com/powervisiontz ) ;

INAKULETEA UZINDUZI WA ALBUM YA QASWIDA ZA ''MAZAUG'' NDANI YA MKOA WA KILIMANJARO, SIKU YA SIKUKUU YA EID MOSI - MWAKA HUU 2014!

UZINDUZI HUU UTAAMBATANA NA BURUDANI KALI YA '''LIVE'' KUTOKA KWA WANA-MAZAUG WOTE::::::

USHAPATA PICHA HAPO??

YAAAAANIIIIIIIIII.................ITAKUWA HIVI;

ZITAIMBWA QASWIDA ZOTE TANO (5) PAMOJA NA KUONESHWA VIDEO ZAKE KWENYE SKRINI KUBWA ZITAKAZOKUWEPO!

PIA KUTAKUWA NA FURSA YA KUPIGA PICHA NA WASANII WA MAZAUG....

KAENI MKAO WA KUBURUDANIKA WAKAZI WA KILIMANJARO (UGWENO), KWANI HII ITAKUWA NI ZAIDI YA HISTORIA ! ! !

ENDELEA KUFUATILIA TAARIFA ZAIDI KUTOKA HAPA KWENYE PAGE YETU TUTAENDELEA KUKUJUZA ZAIDI.............


Friday, 11 July 2014

MJUE FAIZ NA VITU AVIPENDAVYO


Naitwa Fadhili Massanza nina umri wa miaka 29 mzaliwa wa Kilimanjaro Mwanga - Ugweno. mwenyeji wa Dar es saalam - Ilala - Buguruni Mnyamani. 

Napenda sana kufanya shughuli zangu ndogondogo na nnapenda sana kuimba (QASWIDA).

Kusikiliza mambo mbalimbali ya kiuchumi na kidini. 

Napenda sana kuishi na watu wa rika tofauti tofauti na wenye upeo mbalimbali kwani huwa ni mwongozo katika maisha yangu hasa pale ninapojifunza na kuyachukuwa mazuri kutoka kwao. 

Napenda vijana wenzangu hasa wenye hari ya kujituma na kuhangaika kwa ajili ya kesho yao na familia zao.

Napenda kutoa nasaha zangu kwa vijana wote wake kwa waume tujitahidi kupambana vita dhidi ya umaskini na ufukara kwani hata Mungu ametuusia kupambana navyo vyote. 

Hakuna njia yeyote kujikwamua zaidi ya kufanya kazi kwa juhudi na pia kuelekeza nguvu na maombi kwa Mungu pekee katika yote tunayo yafanya kwani
 "Mungu humpa amtakaye bila ya hesabu"


Nawapenda nyote RAMADHAN QAREEM